Kiongozi wa kampeni ya kujitoa Nigel Farage amesema siku hii itakumbukwa kihistoria kama siku ya Uhuru.
Wanamgambo wanounga mkono serikali ya Umoja walikamata wilaya mbili ndani ya Sirte.
Dr.Chris Funk anasema inaweza kuathiri mifumo ya muda mrefu ya hali ya hewa hata katika nchi isiyo na bahari .
Makombora hayo mawili yalirushwa mapema Jumatano na inaaminika kuwa ni kombora la masafa ya kati linalojulikana kama Musudan ambalo lina uwezo wa kufikia kambi za kijeshi za Marekani huko Asia na Pacific.
Tuna chama ambacho ninamaanisha kwamba ninapata shida zaidi na watu waliomo humo kuliko ninavyopata taabu na wademokrat-Trump.
Wanamichezo wa Kenya wanakabiliwa na changamoto sawa na Russia-Thomas Bach.
Mshambuliaji wa Orlando alijitangaza kuwa ni mwanamgambo wa kiislam-FBI.
Mapendekezo yote yameshindwa kupata uungaji mkono wa tatu ya tano inayohitajika ili kuweza kupitishwa.
Kwa wanaharakati wa mazingira mwaka wa 2015 ulikuwa ni mwaka wa hatari kulingana na ripoti kutoka shirika la ufwatiliaji la Global Witness.
Ingawaje kunasa nishati kutokana na miale ya jua kunahitaji mtaji mkubwa, hilo litawezekan kwa bei nafuu kwa kutumia teknologia mpya.
Korea Kusini inachukua hatua za kuongeza usalama ili kuzuia uwezekano wa shambulizi kutoka Islamic State (IS) baada ya Idara ya Ujasusi ya nchi hiyo kuonya kwamba kundi hilo la kigaidi huwenda linalenga vituo vya kijeshi vya Marekani pamoja na raia kwenye peninsula ya Korea.
Makundi ya kutetea Haki za Binadamu yanatoa wito kwa Jumuia ya Mataifa ya Kusini Mashariki mwa Asia (ASEAN) kuchukua juhudi zaidi katika kuwapatia makazi kiasi cha wakimbizi 7,000 waislam wa Myanmar, mwaka mmoja baada ya wakimbizi hao kuokolewa baada ya kuachwa baharini na wasafirishaji biashara haramu.
Wabunge wa Croatia wamepiga kura leo Jumatatu kutaka kuvunjwa kwa bunge na kutoa njia ya uchaguzi mpya unaotarajiwa kufanyika mwanzoni mwa mwezi Septemba.
Timu hii imeweka historia kuwa ya kwanza kushinda baada ya kuwa nyuma kwa jumla ya michezo 3-1 katika fainali za NBA.
Sanduku la kwanza la takwimu kutoka ndege namba M804 ambayo ilikuwa ikielekea Cairo kutoka Paris lilionekana siku moja kabla.
IS iliuteka mji wa Fallujah mwaka 2014, lakini baada ya mapambano makali zaidi ya mwezi uliopita, vikosi vya Iraq vimeweza kuuteka tena takribani nusu ya mji.