Burundi - Voice of America http://www.voaswahili.com/archive/burundi/latest/2772/4661.html Burundi http://www.voanews.com/img/voa/rssLogo_VOA.gif Burundi - Voice of America http://www.voaswahili.com/archive/burundi/latest/2772/4661.html sw 2012 - VOA 60 Wed, 12 Oct 2016 03:42:58 +0300 Pangea CMS – VOA Samsung yasitisha kabisa utengenezaji wa Galaxy Note7 Kampuni  kubwa ya vifaa vya  elektronki ya Samsung iliyoi na makao yake makuu Korea Kusini, ilisema siku ya Jumanne kuwa haitatengeneza tena  simu aina ya Galaxy Note 7 kutokana na matatizo yaliyojitokeza kufuatia ripoti kadhaa kote ulimwenguni kuhusu kupata joto sana  kwa simu hiyo.  L Kampuni hiyo ilitangaza kufunga kabisa utengenezaji kwa maslahi ya usalama wa mnunuzi.  Samsung awali ilitangaza  kwamba inasitisha mauzo yote ya galaxt note 7 kote ulimwenguni  na kuwashauri wateja wake kuacha  haraka kutumia kifaa hicho. Samsung imepata hasara ya asilimia 8 katika hisa zake katika soko la hisa wakati wa kufunguliwa kwa biashara hivi leo. Makampuni kadhaa makubwa ya simu za mkononi ikiwemo kampuni ya AT & T yenye makao yake hapa marekani na ya ujerumaini ya T-Mobile kila moja imetangaza jumapili kuwa imesitisha mauzo  au kubadilisha  simu ya galaxy note 7.   http://www.voaswahili.com/a/samsung-halts-galaxy-note7-production/3545565.html http://www.voaswahili.com/a/samsung-halts-galaxy-note7-production/3545565.html Tue, 11 Oct 2016 17:34:40 +0300 HabariAfrikaMarekaniDuniaTanzaniaKenyaUgandaJamhuri ya Kidemokrasia ya kongoBurundiRwanda Burundi yawazuia wachunguzi wa UN kuingia nchini humo Serikali ya Burundi imewapiga marufuku wachunguzi wa kitengo kinachoshughulika na masuala ya haki za binadamu katika Umoja wa Mataifa kuingia nchini humo kufuatia kutolewa kwa ripoti ambayo inaeleza ukiukwaji mbaya wa haki za binadamu katika nchi hiyo iliyopo Afrika mashariki. Kwa mujibu wa shirika la habari la Associated Press-AP barua iliyotolewa Jumatatu iliyotiwa saini na waziri wa mambo ya nje wa Burundi, Alain Aime Nyamitwe, ilisema wachunguzi wa Umoja wa Mataifa, Pablo de Greiff raia wa Colombia, Christof Heyns wa Afrika kusini na Maya Sahli-Fadel wa Algeria hawaruhusiwi kuingia nchini humo. Wachunguzi hao kutoka kitengo kinachohusika na masuala ya haki za binadamu katika Umoja wa Mataifa wanahusishwa na ripoti iliyotolewa mwezi uliopita ambayo inawashutumu maafisa wa serikali ya Burundi kwa ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu unaowalenga wapinzani wa serikali. Msemaji wa Umoja wa Mataifa, Stephane Dujarric, alizungumza huko New York nchini Marekani na alitoa wito kwa Burundi kuendelea kushirikiana na wachunguzi hao wa haki za binadamu. http://www.voaswahili.com/a/burundi-yawazuia-wachunguzi-wa-un-kuingia-nchini-humo/3545149.html http://www.voaswahili.com/a/burundi-yawazuia-wachunguzi-wa-un-kuingia-nchini-humo/3545149.html Tue, 11 Oct 2016 04:53:44 +0300 HabariAfrikaBurundi