Dunia - Voice of America http://www.voaswahili.com/archive/dunia/latest/2772/2783.html Idhaa ya kiswahili ya  Sauti ya Amerika, tuna vipindi juu ya masuali mbali mbali, pamoja na habari na muziki. http://www.voanews.com/img/voa/rssLogo_VOA.gif Dunia - Voice of America http://www.voaswahili.com/archive/dunia/latest/2772/2783.html sw 2012 - VOA 60 Tue, 20 Sep 2016 00:17:20 +0300 Pangea CMS – VOA Ruto akosoa jamii ya kimataifa kuhusu Daadab Na BMJ Muriithi Naibu wa rais wa Kenya, William Ruto, siku ya Jumatatu aliikosoa jamii ya kimataifa kwa kile alichokiita ukosefu wa uwajibikaji kuhusiana na mzozo wa wakimbizi barani Afrika. Akizungumza wakati wa mkutano wa viongozi wa nchi na serikali uliofanyika katika ukumbi wa umoja wa Mataifa mjini New York, Marekani, Ruto alisema kuwa Kenya imeonyesha ukarimu mwingi kwa wakimbizi walio kwenye kambi ya Daadab, na kwamba sasa ni wakati mwafaka kwao kurejea makwao. Ruto alikuwa mmoja wa waliozungumza katika kikao kilichoitishwa kwa minajiri ya kutafuta suluhisho la kudumu kwa mzozo wa uhamaji wa halaiki ya wakimbizi kutoka maeneo yaliyokumbwa na vita na migogoro ya kisiasa, zikiweno nchi za Syria na Somalia. Alisema msimamo wa kenya wa kuwahamisha wakimbizi hao hautabadilika na kuhoji ni kwa nini mikutano ya viwango vya juu kuhusu swala la wakimbizi hufanyika na ili hali mengi ya mataifa ya yanayoahidi kutoa misaada hayatimizi ahadi hizo. Alitaja changamoto zinalzoletwa nauhifadhi wa wakimbizi kama vile ukosefu wa usalama na kusema kuwa shambulizi la kigaidi la miaka mitatu iliyopita - Westgate - lilipangwa katika kambi ya Daadab. Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki Moon, alizitaka serikali za nchi wanachama ywa umoja huo, kuonyesha nia ya dhati ya kukabiliana na mzozo wa wakimbizi ambao, alisema, umefika viwango vibaya zaidi tangu vita vya pili vya dunia. kikao cha 71 cha Umoja wa mataifa kilianza Jumatatu na kilitarajiwa kufunguliwa rasmi siku ya Jumanne. Kwa mara ya kwanza kwa muda mrefu, marais wa Kenya, Tanzania na Uganda hawakuhudhuria kongamano la mwaka huu na badala yake kuwatuma wawakilishi. rais wa Uganda Yoweri Museveni yuko ziarani Ufaransa huku mabwana Magufuli na Kenyatta wakisalia nchini mwao mtawalia. http://www.voaswahili.com/a/ruto-says-international-community-should-do-more/3515825.html http://www.voaswahili.com/a/ruto-says-international-community-should-do-more/3515825.html Mon, 19 Sep 2016 23:53:50 +0300 HabariAfrikaMarekaniDunia Aung San Suu Kyi wa Myanmar akutana na Wabunge Marekani Kiongozi wa Myanmar, Aung San Suu Kyi, siku ya Alhamisi  alikutana na viongozi wa bunge la Marekani, siku moja tu baada ya rais Barack Obama kutangaza kuwa serikali yake iko tayari kuondoa vikwazo vya kiuchumi  dhidi ya nchi hiyo. Kwa mujibu wa ratiba rasmi, Aung San Suu Kyi, ambaye yuko ziarani hapa Marekani, alitarajiwa kukutana na kiongozi wa wachache katika bunge la Congress, Nancy Pelosi na kiongozi wa waliowengi katika seneti, Mitch McConnell, na vile vile kuhudhuria dhifa itakayoandaliwa na viongozi wa kibiashara na hatimaye kufanya kikao cha maswali na majibu na wanafunzi wa shule ya upili ya Washington. Huenda pia Aung San Suu Kyi akajaribu kuwashawishi wabunge wenye ushawishi mkubwa bungeni kwamba huu ni wakati mwafaka kuondoa vikwazo hivyo vya kiuchumi dhidi ya nchi yake. http://www.voaswahili.com/a/aung-san-suu-kyi-meets-us-leaders/3510770.html http://www.voaswahili.com/a/aung-san-suu-kyi-meets-us-leaders/3510770.html Thu, 15 Sep 2016 21:59:46 +0300 HabariMarekaniDunia Aleksander Ceferin ndiye Rais mpya wa UEFA Shirikisho la soka la Ulaya UEFA, Jumatano limemteuwa Aleksander Ceferin kutoka Slovenia kuwa Rais wake mpya. http://www.voaswahili.com/a/uefa-president/3509217.html http://www.voaswahili.com/a/uefa-president/3509217.html Wed, 14 Sep 2016 00:00:04 +0300 HabariDunia Kerry awasili Uswizi kwa mazungumzo kuhusu Syria Huku waziri wa mambo ya nje wa Marekani, John Kerry, akiwasili Uswizi siku ya Ijumaa ili kuanza awamu nyingine ya mazungumzo na mwenzake wa Russia, Sergei Lavrov, maafisa wa kidiplomasia wanaoandamana naye walionekana kutokuwa na matumaini makubwa kuhusu makubaliano yaliyotarajiwa ya kusitisha mapigano nchini Syria. Afisa mmoja wa Marekani amenukuliwa akisema kuwa hawawezi kutoa hakikisho lolote kwamba makubaliano hayo yatafua dafu. Lakini Kerry, aliyezungumza kwa njia ya simu na waziri wa mambo ya nje wa Russia, Lavrov, takriban mara nne siku ya Jumatano na jana Alhamisi, alikuwa na matumaini na ndiyo sababu alirudi tena Uswizi kwa kile kinachotarajiwa kuwa mkutano usiozidi siku moja. Kwa siku kadhaa, maswala nyeti yameelezwa nana maafisa wa Marekani kama ya kiufundi. Moja ya maswala hayo, ni kuhakikisha kwamba mji wa Aleppo hautazingirwa tena. http://www.voaswahili.com/a/kerry-arrives-in-swaitzerland/3500125.html http://www.voaswahili.com/a/kerry-arrives-in-swaitzerland/3500125.html Fri, 09 Sep 2016 15:19:05 +0300 HabariMarekaniDunia Russia na Marekani wana maslahi ya pamoja ya kuishinda Islamic State-Trump Trump amsifu rais Putin kuwa kiongozi bora kuliko Obama. http://www.voaswahili.com/a/russia-marekani-trump-clinton-isis/3498855.html http://www.voaswahili.com/a/russia-marekani-trump-clinton-isis/3498855.html Thu, 08 Sep 2016 17:47:00 +0300 HabariMarekaniDunia Rais wa Ufilipino ajutia matamshi yake kwa Obama Rais wa Ufilipino, Rodrigo Duterte ameelezea kusikitishwa na matamshi yake yaliyohusisha lugha chafu  na kutoa taswira ya kumshambulia rais Barack Obama wa Marekani. Katika taarifa yake ameeleza kwamba lengo lao la msingi ni kuweka sera ya kimataifa ya kujitegemea wakati wakihamasisha uhusiano wa karibu na mataifa yote hasa Marekani ambayo imekuwa na ushirikiano wa muda mrefu. Kabla ya kuondoka Jumatatu kuelekea katika mkutano wa kikanda huko Laos, Duterte alimuonya rais Obama kutomfundisha namna ya kupambana na wasafirishaji wa dawa za kulevya. Mapambano hayo yamesababisha vifo vya zaidi ya watu 2,000 toka alipoingia madarakani mwezi Juni. Kufuatia kauli za rais huyo wa Ufilipino, rais Barack Obama alifuta mkutano wake uliokuwa umepangwa na badala yake atakuwa na mkutano na kiongozi wa Korea Kusini. http://www.voaswahili.com/a/rais-wa-ufilipino-ajutia-matamshi-yake-kwa-obama/3496809.html http://www.voaswahili.com/a/rais-wa-ufilipino-ajutia-matamshi-yake-kwa-obama/3496809.html Wed, 07 Sep 2016 04:55:00 +0300 HabariMarekaniDunia Wasomali walio nje watakiwa kurudi Somalia Rais wa Somalia, Hassan Sheikh Mohamud anasema anawataka Wasomali zaidi vijana waliopo nje ya nchi kurejea nyumbani. Kurejea kwao ni kusaidia kuijenga nchi licha ya kwamba wanamgambo wa Al-Shabab wanaendelea na mashambulizi hatari. Rais Mohamud aliongea na VOA mjini Mogadishu na kujibu maswali kuhusu masuala mbalimbali katika mkutano uliofadhiliwa na VOA siku ya Jumamosi. Tukio hilo lilikuwa la kwanza la kipekee kuunganisha Mogadishu mji mkuu wa Somalia, na mji wa St. Paul, jimboni Minessota,  ambapo kuna jumuiya kubwa zaidi ya Wasomali nchini Marekani. Rais huyo alisema Wasomali waliopo nje ya nchi wamehusika katika mfumuko wa biashara nyingi nchini hasa mji mkuu wa Somalia, toka kuondoka kwa kundi la Al-Shabab mji humo mwaka 2011. http://www.voaswahili.com/a/wasomali-walio-nje-watakiwa-kurudi/3496806.html http://www.voaswahili.com/a/wasomali-walio-nje-watakiwa-kurudi/3496806.html Wed, 07 Sep 2016 04:48:50 +0300 HabariAfrikaDunia WHO yabadilisha muongozo wa Zika Shirika la afya duniani (WHO) linabadilisha ushauri wake kuhusu virusi vya Zika, likiwaeleza wasafiri kwamba yoyote ambaye ametembelea sehemu  inayokabiliana na mlipuko huo kufanya ngono salama ama kuacha kufanya mapenzi kwa miezi sita. Shirika hilo la afya la umoja wa mataifa lilitoa muongozo huo mpya hapo Jumanne, likirekebisha  muongozo wa mwezi Juni ambao iliwashauri wanaume kufanya ngono salama ama kuacha kabisa kufanya mapenzi kwa wiki nane baada ya kutembelea nchi iliyoathiriwa na Zika. Maboresho hayo yanakuja wakati uthibitisho zaidi ukizuka na kuonyesha namna mbu wanao ambukiza Zika wanaweza kuambukizwa kwa baina ya mtu na mtu. http://www.voaswahili.com/a/whoyabadilisha-muongozo-wa-zika/3496804.html http://www.voaswahili.com/a/whoyabadilisha-muongozo-wa-zika/3496804.html Wed, 07 Sep 2016 04:42:59 +0300 HabariAfrikaDunia Baraza la Uslama la UM kujadili makombora ya Korea Kaskazini Wanadiplomasia wanasema baraza la usalama la Umoja wa Mataifa linakutana leo kujadili majaribio ya karibuni ya makombra ya  Korea Kaskazini. Korea Kaskazini imesha fyatua makombora matatu katika bahari ya Japan Jumatatu kutoka katika jimbo la Hwanghae, lililopo katika  mwambao wa mashariki wa nchi hiyo. Mkuu wa majeshi ya muungano ya Korea Kusini ameyataja makombora hayo kama makombora ya Rodong, yenye uwezo wa kusafiri umbali wa  kilometa 1,000. Wizara ya ulinzi ya Japan inasema makombora hayo yalidondoka katika ukanda wa mahsusi wa kiuchumi katika eneo hilo ambalo linajulikana kama bahari ya mashariki. Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imesema majaribio ya makomboroa ya  Korea kaskazini yamekuwa ya kawaida sana katika miezi kadhaa iliyopita. http://www.voaswahili.com/a/baraza-la-usalama-la-um-lagawanyika/3495272.html http://www.voaswahili.com/a/baraza-la-usalama-la-um-lagawanyika/3495272.html Tue, 06 Sep 2016 05:24:14 +0300 HabariDunia Rais Obama ahutubia Mataifa ya South Pacific Rais Barack Obama wa Marekani Jumanne alihakikishia mataifa yalioko kwenye eneo la Asia Pacific usaidizi wa Marekani. http://www.voaswahili.com/a/obama-south-pacific/3495923.html http://www.voaswahili.com/a/obama-south-pacific/3495923.html Tue, 06 Sep 2016 00:00:28 +0300 HabariDunia Trump amkaribia Clinton kwa maoni ya umma Wachambuzi kadhaa wa kisiasa bado wanabashiri Clinton atakuwa rais wa 45 wa Marekani na mkuu wa kwanza wa majeshi mwanamke. http://www.voaswahili.com/a/clinton-trump-uso-kwa-uso-mdahalo/3493845.html http://www.voaswahili.com/a/clinton-trump-uso-kwa-uso-mdahalo/3493845.html Mon, 05 Sep 2016 06:38:08 +0300 HabariMarekaniDunia Mama Teresa atangazwa kuwa mtakatifu Misa ya kutangazwa mama Teresa mtakatifu ilikuwa muhimu kwa watu wengi duniani kote http://www.voaswahili.com/a/mama-teresa-mtakatifu-kanisa-katoliki/3493815.html http://www.voaswahili.com/a/mama-teresa-mtakatifu-kanisa-katoliki/3493815.html Mon, 05 Sep 2016 04:38:42 +0300 HabariDunia Trump asisitiza Mexico italipia ujenzi wa ukuta Mwenyekiti wa kampeni ya Clinton John Podesta amema Trump amejikaba mwenyewe kwa kutokuzungumzia suala hilo kwa ukamilifu na rais Pena Nieto. http://www.voaswahili.com/a/trump-uhamiaji-hotuba-mexico-arizona/3489415.html http://www.voaswahili.com/a/trump-uhamiaji-hotuba-mexico-arizona/3489415.html Thu, 01 Sep 2016 14:53:39 +0300 HabariMarekaniDunia Vifo kutokana na shambulizi la jumanne Somalia vimeongezeka Maafisa wa Somalia wanasema idadi ya vifo kutokana na bomu lililotegwa kwenye gari jumanne karibu na makazi ya rais imeongezeka kufikia vifo visivyopungua 22 baada ya majeruhi kadhaa kufariki kutokana na majeraha waliyoyapata. Gari liligonga ukuta wa hoteli ya SYL, eneo maarufu la mikutano kwa maafisa wa serikali ya Somalia. Mkuu wa kitengo cha gari la kubeba wagonjwa katika eneo, Dr.Abdulkadir Aden, anasema kitengo chake kilisafirisha maiti 22 na majeruhi 30 baada ya mlipuko. Miongoni mwa watu hao waliokufa sita walikuwa wanawake. Afisa wa polisi mjini Mogadishu, Meja Mohamed Abdullah aliliambia shirika la habari la Reuters kwamba watu 50 walijeruhiwa katika shambulizi hilo. Miongoni mwa waliojeruhiwa katika mlipuko huo walikuwa waziri wa usafiri, waziri wa ulinzi, wabunge kadhaa na waandishi wa habari wawili wa redio kutoka kwenye eneo. http://www.voaswahili.com/a/vifo-kutokana-na-shambulizi-la-jumanne-mogadishu-vimeongezeka/3487830.html http://www.voaswahili.com/a/vifo-kutokana-na-shambulizi-la-jumanne-mogadishu-vimeongezeka/3487830.html Wed, 31 Aug 2016 15:11:40 +0300 HabariAfrikaDunia Kamati ya kutatua mzozo kwenye bunge la Liberia yabuniwa Rais wa muda wa baraza la Seneti la Liberia amesema Jumatatu kuwa baraza lake limebuni kamati ya muda ili kujaribu kusuluhisha mvutano kwenye baraza la wawakilishi. http://www.voaswahili.com/a/liberia-senate-stalemate/3484946.html http://www.voaswahili.com/a/liberia-senate-stalemate/3484946.html Mon, 29 Aug 2016 00:00:20 +0300 HabariAfrikaDunia Nyumba ya 'Prince' kufunguliwa kwa maonyesho Kampuni ya Bremer Trust ilitangaza kwamba washabiki wake wanaweza kununua tiketi kwenye mtandao kuanzia Ijumaa. http://www.voaswahili.com/a/prince-nyumba-maonyesho-mirathi/3480505.html http://www.voaswahili.com/a/prince-nyumba-maonyesho-mirathi/3480505.html Thu, 25 Aug 2016 18:41:47 +0300 HabariMarekaniDunia Idadi ya vifo Italia yafikia 247. Maafisa wa Italia wamesema idadi ya vifo kutokana na  tetemeko la ardhi la Jumatano imeongezeka na kufikia 247. Idara ya kulinda raia ya Italia imetangaza idadi mpya Jumatano jioni kutoka idadi ya mwanzo ya watu 124. Waokozi wanaendelea kutafuta waathirika mpaka usiku ambao wamefukiwa na vifusi. Mapama Jumatano, waziri mkuu, Matteo Renzi alisafiri kwa helkopta kwenda maeneo yaliyoathirika na kuwafariji  waokozi wa kujitolea. Renzi pia aliongea na waziri wa miundombinu na mkuu wa idara ya uliznzi wa raia. Tetemeko la ardhi lilipiga  eneo moja nchini humo majira ya saa tisa na nusu alfajiri kwa saa za huko na kusababisha uharibifu mkubwa katika miji mitatu karibu na kiini  cha tetemeko. Watoto ni miongoni mwa waliopoteza maisha. http://www.voaswahili.com/a/idadi-ya-vifo-italia-yafikia-159/3480037.html http://www.voaswahili.com/a/idadi-ya-vifo-italia-yafikia-159/3480037.html Thu, 25 Aug 2016 04:42:19 +0300 HabariDunia Mataifa ya Afrika yanazidi kudidimiza matumizi ya mitandao Ripoti kutoka Burundi zinasema polisi wamewakamata watu wanane siku ya Jumamosi kwa shutuma za kusambaza taarifa za kupinga serikali kwenye mtandao. Hatua hiyo ya Burundi sio jambo geni barani Afrika. Orodha ya mataifa ya Afrika yanayojaribu kuzuia au kudhibiti mitandao ya kijamii inaongezeka hususan katika kipindi cha uchaguzi. Henry Mhina, mkurugenzi wa jarida la Article 19 la Afrika Mashariki, taasisi ambayo inatetea uhuru wa kujieleza anasema serikali katika eneo hilo bado zinadidimiza uhuru wa kujieleza. Zimbabwe hivi karibuni ilianza kutumia sheria ya mwaka 2002 inayokataza  kumtusi rais ili kuwakamata watu kwa taarifa walizozitoa kwenye mitandao ya kijamii. Nchi ya Angola ilibuni “Angola Social Communication Regulatory Body” inayoendeshwa na chama tawala ili kuhakikisha inadhibiti sheria mpya ya vyombo vya habari. Wakati huo huo mataifa mengine barani Afrika kama Mali ilifungia mitandao ya kijamii mjini Bamako mwezi wa nane kufuatia kukamatwa kwa mwandishi wa habari maarufu kwenye redio baada ya kukamtwa kwake kusababisha ghasia za waandamanaji ambapo watu kadhaa waliripotiwa kuuwawa. Nayo serikali ya Uganda ilizuia fursa kwa mitandao ya kijamii kusambaza taarifa wakati wa uchaguzi mkuu wa urais uliofanyika Februari mwaka 2016 na tukio hilo kujirudia tena wakati wa kuapishwa kwa Rais Yoweri Museveni ambaye amekuwepo madarakani kwa muda mrefu nchini humo. Lakini Waganda wengi waliweza kupata taarifa za kile kinachoendelea nchini mwao kupitia mtandao binafsi au VPN. Katika ripoti ya mwaka 2015 ya Privacy International ilielezea kwa kina matumizi ya kiupelelezi yaliofanywa na polisi na jeshi nchini Uganda ili kufuatilia wafuasi wanaoongoza upinzani, wanaharakati, maafisa waliochaguliwa, wapelelezi walioko ndani ya mfumo wa kazi pamoja na waandishi wa habari kufuatia uchaguzi wa mwaka 2011. Serikali ya Uganda ilikanusha shutuma hizo na kukataa kufanyika uchunguzi bungeni juu ya suala hilo. http://www.voaswahili.com/a/mataifa-ya-afrika-yanazidi-kudidimiza-matumizi-ya-mitandao/3479403.html http://www.voaswahili.com/a/mataifa-ya-afrika-yanazidi-kudidimiza-matumizi-ya-mitandao/3479403.html Wed, 24 Aug 2016 23:08:58 +0300 HabariAfrikaDunia Somaliland yataka kutambuliwa kimataifa kama nchi Zaidi ya raia milioni moja wametia sahihi wakitoa wito wa kutambuliwa Somaliland na jumuiya ya kimataifa, Rais wa Somaliland Ahmed Mohamed Silanyo aliwaambia waandishi wa habari Jumanne huko Hargeisa. Somaliland ilijitenga kutoka Somalia mwaka 1991 baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe vya miaka mitatu. Eneo hilo tangu wakati huo linajiendesha kwa mamlaka yake yenyewe, lakini hakuna taifa lolote limetambua uhuru wake. Katika kujibu ombi hilo Somalia imerudia tena wito wa kutaka kuungana. Maafisa wa Somaliland walisema wamekusanya sahihi kutoka kwa nwatu milioni moja kutoka maeneo sita ya Somaliland tangu mwezi April.   Waziri wa mambo ya nje wa Somaliland, Sa’ad Ali Shire aliiambia sauti ya Amerika kwamba mtu atasoma taarifa inayotoa wito wa kutambuliwa Somaliland. Kama hawawezi kusoma mtu mwingine atawasomea. Somaliland ina sarafu yake yenyewe, jeshi na katiba iliyopigiwa kura kufuatia kura ya maoni mwaka 2001. Bwana Shire alisema sahihi hizo zitapelekwa kwa viongozi wa kimataifa wakiwemo Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika. Serikali ya Somalia wakati wote inasisitiza Somaliland ni sehemu ya Somalia.   http://www.voaswahili.com/a/somaliland-yataka-kutambuliwa-kimataifa-kama-nchi/3478664.html http://www.voaswahili.com/a/somaliland-yataka-kutambuliwa-kimataifa-kama-nchi/3478664.html Wed, 24 Aug 2016 15:22:38 +0300 HabariAfrikaDunia Tetemeko kubwa la ardhi latikisa Italia na kuua watu kadhaa Tetemeko kubwa la ardhi lilitokea kati kati ya Italy mapema Jumatano na kusababisha uharibifu mkubwa kwenye maeneo karibu na makutano ya miji na kuuwa watu wasiopungua 39. Idara ya hali ya hewa ya marekani imetaja tetemeko la kiwango cha 6.2 rikta kilichoanzia kwenye makutano ya kiasi cha kilomita 10 kusini-mashariki mwa mji wa Norcia. Mtikisiko ulikumba sehemu kubwa ya eneo ikiwemo mji mkuu, Rome uliopo umbali wa kilomita 150. Mtetemeko ulianza baada ya saa tisa na nusu alfajiri kwa saa za huko na kufuatiwa na mitetemeko kadhaa baada ya hapo.  Idara ya kiraia ya kulinda majanga nchini Italy imesema watu kadhaa walijeruhiwa na wengi wanahitaji msaada wa makazi ya muda.  http://www.voaswahili.com/a/tetemeko-la-ardhi-latikisa-italia/3478665.html http://www.voaswahili.com/a/tetemeko-la-ardhi-latikisa-italia/3478665.html Wed, 24 Aug 2016 15:18:32 +0300 HabariDunia