Jumatatu, Machi 28, 2016 Local time: 16:14
Sauti
Multimedia
 Kanda
 Katika Picha
 YouTube

    Habari

    Uchaguzi wa marudio wa Zanzibar kufanyika Jumapili

    Uchaguzi huo unafanyika baada ya mwenyekiti wa tume ya uchaguzi ya Zanzibar Jecha Salim Jecha kufuta uchaguzi uliofanyika Oktoba 25 mwaka jana kwa madai kuwa kulikuwapo na dosari kadhaa.

    Vijana wanaounga mkono upinzani wakiimba na kucheza katika uchaguzi wa octoba, 2015

    Uchaguzi wa marudio wa urais, madiwani na wawakilishi huko Zanzibar unatarajiwa kufanyika Jumapili Machi 20, 2016.

    Uchaguzi huo unafanyika baada ya mwenyekiti wa tume ya uchaguzi ya Zanzibar Jecha Salim Jecha kufuta uchaguzi uliofanyika Oktoba 25 mwaka jana kwa madai kuwa kulikuwapo na dosari kadhaa.

    Imeelezwa kwamba uchaguzi huo utafanyika na kushirikisha chama cha mapinduzi -CCM na vyama vingine vidogo baada ya chama cha wananchi CUF kususia na kudai hakukuwa na sababu ya kufuta uchaguzi wa awali.

    Sam Kiboma na Faith Bilal ni wakaazi wa Zanzibar wametoa maoni yao.

    Uchaguzi Zanzibar
    uchaguzi zanzibari
    ▶ || 0:00:00
    ... ⇱  
    • MP3 - 553.9kB
    • MP3 - 554.1kB
     
     
    X

    Wiki hii kumekukuwepo na taarifa za matukio ya kuhatarisha usalama lakini jeshi la polisi limesema limejipanga kukabiliana na kila hali.

    You May Like

     Ujumbe wa Pasaka wa Rais J. Magufuli wa Tanzania

    Rais John Magufuli wa Tanzania ahudhuria misa ya Pasaka na kutoa ujumbe wa watu kufanya kazi kwa bidi kuleta maendeleo nchini mwao. Zaidi

    Mji wa kale wa Syria, Palmyra wakombolewa

    Ndege za kivita za Russia zimefanya takriban mashambulizi elfu moja ya anga katika juhudi za kutorosha wapiganaji wa Islamic State kutoka Palmyra. Zaidi

     Waandamanaji wa mrengo wa kulia washambulia waombolezi Brussels

    Polisi wa kupambana na ghasia huko Ubelgiji wametumia mabomba ya maji kuwatawanya wanaharakari wa itikadi kali za mrengo wa kulia wanaopinga wahamiaji walopambana na waombolezi, wa mashambulizi ya kigaidi. Zaidi

    Watu 30 wauwawa Iraq na wengine 80 kujeruhiwa

    Watu 30 wameuwawa baada ya mshambuliaji kuvamia uwanja wa mpira wa miguu nchini Iraq na kutegua milipuko yake. Wengine 80 wamejeruhiwa vibaya katika shambulizi hilo Ijumaa Zaidi

     Ziara ya Obama nchini Argentina

    Rais Barack Obama atembelea Argentina wakati nchi hiyo inaadhimisha miaka 40 tangu mapinduzi yaliyoweka madarakani utawala wa kijeshi ulitenda ukatili dhidi ya raia wake. Zaidi

    Zaidi Marais wa Afrika wamekaa madarakani kwa muda gani?