Jumatatu, Machi 28, 2016 Local time: 12:05
Sauti
Multimedia
 Kanda
 Katika Picha
 YouTube

    Habari / Afrika

    Tanzania na Kenya kushirikiana kiuchumi

    Viongozi wa Tanzania na Kenya wamekubaliana kushirikiana katika masuala ya uchumi ili kuboresha miradi ya maendeleo na miundo mbinu.

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli amefanya mazungumzo na rais wa Jamhuri ya Kenya, Uhuru Kenyatta, kando ya mkutano mkuu wa 17 wa kawaida wa wakuu wa nchi wa jumuiya ya Afrika Mashariki na wawili hao kukubaliana kuboresha mahusiano hasa katika nyanja ya kiuchumi.

    Miongoni mwa masuala wanayotarajia kutiliwa mkazo ni pamoja na kutekeleza miradi ya maendeleo inayohusisha nchi hizo mbili hasa katika ujenzi wa miundo mbinu, kukuza biashara na kuzalisha ajira kupitia viwanda.

    Kwa upande wake rais Kenyatta wa Kenya amesema amefurahi kwa kuona rais wa Tanzania yuko tayari kuimarisha uhusiano wa nchi hizo mbili ambao utasaidia katika kumaliza umaskini na kukuza uchumi.

    Marais wengine waliohudhuria mkutano huo ni pamoja na Paul Kagame wa Rwanda, Yoweri Museveni wa Uganda na makamu wa rais wa Burundi anayemuakilisha rais wa nchi hiyo, Pierre Nkurunzinza.

    Waliokuwa wamealikwa katika mkutano huo ni pamoja na viongozi mbalimbali, akiwemo rais wa Sudan kusini, Salva Kiir, aliyewakilishwa na Makamu wake wa rais.

    You May Like

    Alfajiri

    Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.

    Jioni

    Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa waandishi wetu sehemu mbali mbali duniani na kote Afrika Mashariki na Kati, na vile vile vipindi na makala maalum kuhusu afya, wanawake, jamii na maendeleo.

    Taarifa ya habari - 5:51

    VOA Express

    VOA Express ni matangazo mapya yenye mwendo wa kasi yakiangalia habari mpya za mchana na maelezo ya maswala yanayohusu vijana na wanawake. Matangazo haya yanafuatilia habari zilizojitokeza nyakati za mchana na ripoti za kina za habari ambazo hazisikiki sana katika matangazo mengineyo. VOA Express pia inafuatilia kwa karibu sana maswala yanayovuma katika mitandao ya kijamii kama sehemu moja muhimu ya upashanaji habari siku hizi.

    Comment on this forum
    Maoni
         
    Hakuna mtu ameandika maoni hapa. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.

    Zaidi Marais wa Afrika wamekaa madarakani kwa muda gani?